Exodus 30:1-4
Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba
(Kutoka 37:25-28)
1 a“Tengeneza madhabahu kwa mbao za mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba. 2 bMadhabahu hayo yawe mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, ▼▼Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.
 na kimo cha dhiraa mbili, ▼▼Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.
 nazo pembe zake zitakuwa kitu kimoja nayo.  3 eFunika hayo madhabahu juu na pande zote na pia pembe zake kwa dhahabu safi, na uifanyizie ukingo wa dhahabu kuizunguka.  4 fTengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, ziwe mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko itumikayo kuibebea madhabahu.  
    Copyright information for
    SwhNEN
 
