13aBadala ya kichaka cha miiba itaota miti ya misunobari, na badala ya michongoma utaota mhadasi. ▼
▼Mhadasi ni aina ya mti ambao huota milimani karibu na Yerusalemu, hutoa harufu nzuri itumikayo kutengeneza manukato; kwa Kiebrania ni “hadas”, na ilikuwa inatumika kujenga vibanda wakati wa Sikukuu ya Vibanda (ona pia Neh 8:15).
Hili litakuwa jambo la kumpatia Bwana jina, kwa ajili ya ishara ya milele, ambayo haitaharibiwa.”